HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2016

BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR YATOA DAWA KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA.

 Wafanyakazi wa Bohari kuu wakisambaza dawa katika Hospitali ya Wilaya Makunduchi ikiwa ni jitihada za serikali kuwapatia wananchi huduma hiyo bila malipo.
 Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akimkabidhi dawa  Daktari msaidizi wa Hospitali ya Wilaya  Makunduchi Asha Salum Hassa (wa pili kulia) kwa ajili ya Hospitali hiyo.
 Shehena ya dawa zilizoagizwa na S erikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwa zimehifadhiwa kwenye Bohari kuu Maruhubi kabla ya kusambazwa katika hospitali na vituo vya Afya.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha kwamba Hospitali na Vituo vyote vya afya vinapatiwa dawa zote muhimu kwa ajili ya wananchi.

Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamada amesema Serikali tayari imeidhinisha  shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kununulia dawa na Wizara imeshatumia shilingi milioni 600  kununua dawa ambazo zitatosha katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shilingi bilioni tano kwa ajili ya kununulia dawa ambazo zinakidhi  mahitaji ya wananchi katika kuendeleza azma ya Serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bila malipo.

“Hakuna haja ya kuweka akiba dawa wapeni wananchi, dawa zipo zakutosha na utaratibu wa kuagiza nyengine umeshaanza, ”alisisitiza Mkurugenzi wa Bohari Kuu.

Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Makunduchi Dkt.  Asha Salum Hassan amesema hali ya dawa hivi sasa inaridhisha na dawa nyingi muhimu zinapatikana isipokuwa dawa za maumivu na Anti biotic zinatumika kwa wingi hivyo baadhi ya wakati zinakwisha bila ya kuingizwa nyengine.

Ameahidi kuwa dawa hizo zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya wananchi  na atahakikisha kuwa hakutatokea ubadhirifu wowote ulio nje ya utaratibu uliopangwa na Wizara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad