Mtaa Kwa Mtaa Blog

TUZO ZA MAKAMPUNI 100 YA KIWANGO CHA KATI NCHINI KUTOLEWA LEO

Tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini kutolewa leo katika hafla itakayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City. Hayo yamebainishwa katika mkutano uliowakutanisha wadau wote walioshiriki katika mchakato huo pamoja na waandaaji na wadhamini uliofanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Mchakato huu uliratibiwa na KPMG na Mwananchi Communications Ltd na kudhaminiwa na Benki M.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maeneo maalum ya uwekezaji nchini (EPZA) Kanali Mstaafu. Joseph Simbakalia akizungumza na wadau wa tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini katika mkutano wa wadau uliofanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency.Hafla ya ugawaji tuzo hizo itafanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sumaria Group Bwn Ankush Shah, Mkurugenzi mtendaji wa Research Solution Africa Bwn Jasper Grosskurth, Mkurugenzi mkuu wa Institute of Directors Bwn Said Kambi na mwendeshaji wa shughuli hiyo Taji Liundi.
Mkurugenzi Mkuu mteule wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso akizungumza katika mkutano huo, Benki M ndio wadhamini wakuu wa mchakato huo unaoratibiwa na KPMG na Mwananchi Communications Ltd.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget