Mtaa Kwa Mtaa Blog

RC Sadick aiomba Kambi tiba ya GSM Foundation kurudi tena mkoani Kilimanjaro

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq ameiomba taasisi ya GSM Foundation kurudi tena mkoani humo na kuendesha kambi tiba nyingine ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kutimiza lengo la kutibu watoto zaidi ya 50 walioko vijijini ambeo wamechelewa kufikiwa na taarifa ya kambi hiyo.

Ombi hilo amelitoa mbele ya Kaimu mkuu wa kambi tiba ya GSM, Dk. Lemeri Mchome kutoka Taasisi ya  Mifupa na upasuaji ya Muhimbili MOI,  wakati mkuu huyo wa mkoa alipokuwa akikagua maendeleo ya watoto waliofanyiwa upasuaji katka hospitali ya KCMC iliyopo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Sadiq amesema wagonjwa wengi wenye changamoto za tiba wako vijijini na huwachukua siku kadhaa kufika hospitalini hivyo inawezekana wakachelewa kufika kwa wakati kutibiwa na kambi tiba hiyo.

Mpaka sasa kambi tiba hiyo imeshatibia zaidi ya watoto 150 na kuwaona watoto zaidi ya 1000  na imepita katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Songea, Mbeya na Iringa.

Mikoa mingine ambayo imeshafaidika na kambi tiba ya GSM Foundation ni Pwani na Tanga, na sasa kambi iko Mkoani Kilimanjaro ikiendelea na ziara zake ambapo inaelekea Arusha na Mara.
Dk Lemeri Mchome akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadiq
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget