Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia)
akifurahia jambo mara baada ya kupokea msaada wa Shilingi Milioni Kumi
uliyotolewa na Kampuni ya SKOL Bulding Contractors Limited Ofini kwake
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la
ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi Karibuni (Kushoto) ni Bw.Vincent
Massawe kutoka Kampuni hiyo mara baada ya kukabidhi pesa hizo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Building Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kulia) kiasi cha Shilingi Milioni Kumi taslimu leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera waliyoathirika na tetemeko la ardhi liliotokea hivi karibuni.
Na Shamimu Nyaki – WHUSM
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kutoka Kampuni ya Skol Building Contractors Limited.
Akipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Vincent Peter Masawe Waziri Nnauye amemthibitishia kuwa pesa hizo zitawasilishwa kwa waathirika wa tetemeko hilo ili zitatue changamoto zinazowakabili.
“Ninashukuru sana kwa msaada wenu mmetambua changamoto wanazopata wenzetu,niwaombe Watanzania wote tuendelee kujitoa kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa haya”.Alisema Mhe.Nnauye.
Aidha Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw.Vincent Peter Masawe amesema Kampuni yao imeguswa na matatizo waliyopata wakazi hao wa Kagera na ndio maana wameamua kuwasaidia ili hali zao za maisha zireje kama zamani.
“Tumeamua kuwasaidia wenzetu na tunaomba wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla popote walipo waguswe na jambo hili na waunge mkono Serikali katika juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hili”. Aliongeza Bw.Masawe.
Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amewakaribisha wananchi wote katika harambee ya kuchangia waathirika hao iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) itakayofanyika Septemba 21 mwaka huu jioni katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment