HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 9, 2016

MTWARA: MSAFARA WA MAKAMU WARAIS WAPATA AJALI.

Majeruhi wa ajari wakipata msaada wa  huduma ya kwanza mara baada ya gari walilokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka.
Gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Samia Hasan Suluhu jinsi lilivyo haribika mara baada ya Kuacha njia na kupinduka.

 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu Rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad