HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 8, 2016

Kamati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini yatembelea viwanda vya ngozi na nguo jijini mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (wa tatu kushoto) akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayojihusisha na miradi ya pamoja ya ujenzi wa Viwanda, wakati ilipofanya ziara ya kutembelea na kujionea hali halisi ya Viwanda vya ngozi na nguo, jijini Mwanza hivi karibuni. Kamati hiyo inayoundwa na maofisa wataalamu wa uwekezaji na mipango kutoka mifuko yote ya hifadhi ya jamii Nchini, iliongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA), Meshach Bandawe (wa nne kushoto) ambaye ndiye alieratibu Ziara hiyo.
 Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo kilichopo Jijini Mwanza, akitoa ufafanuzi juu mashine za kufumia nguo, kwa wajumbe wa Kamati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayojihusisha na miradi ya pamoja ya ujenzi wa Viwanda, wakati ilipofanya ziara ya kutembelea na kujionea hali halisi ya Viwanda vya ngozi na nguo, jijini Mwanza hivi karibuni.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayojihusisha na miradi ya pamoja ya ujenzi wa Viwanda, wakipatiwa maelezi juu ya namna pamba inavyoweza kuandaliwa mpaka kupatikana nguo.
Mmoja wa Mafundi wa kiwanda cha Ngozi ambacho kinatengeneza viatu vya aina mbalimbali akiendelea na kazi yake.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayojihusisha na miradi ya pamoja ya ujenzi wa Viwanda, wakiangalia Khanga iliyokuwa tayari kutoka kwenye mashine.

Sehemu ya wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad