HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 8, 2016

JOH MAKINI AREJEA COKE STUDIO AFRICA KUSHIRIKIANA NA MSHINDI WA TUZO YA BET FALZ KUTOKA NIGERIA

Msanii mahiri na mfalme wa hip hop Tanzania, Joh Makini aliyetamba na wimbo “Don’t Bother”, yupo Nairobi kwaajili ya kurekodi msimu wa nne na ujao wa kipindi cha Coke Studio Africa. Akirejea kwa mara ya pili kwenye kipindi hicho, Joh ameungana na msanii wa Nigeria na mshindi wa tuzo za BET, Falz The Bahd Guy, mwenye nyimbo zinazofanya vizuri kama “Soft Work”, “Ello Bae” na “Celebrity Girlfriend” akimshirikisha Reekado Banks. Wasanii hao wawili wanatarajiwa kuunganisha ladha za hip hop, pop, R&B, afro-beats, highlife (muziki wenye asili ya Ghana) pamoja na mahadhi mengine na nyimbo zao zitatayarishwa na mtayarishaji mwenye makazi yake Ufaransa, DSK (anayetokea Ivory Coast).

Akiongea kutoka Nairobi wakati wa kurekodi msimu ujao, Joh Makini alisema, “Hadi sasa imekuwa poa sana kufanya kazi na Falz. Tutatengeneza nyimbo kali. Mchanganyiko wa muziki umekuwa na ugumu lakini nimeupenda. Mtayarishaji wetu ametuletea ladha ambazo sikuwahi kuwaza ningekuja kufanya, mashabiki watarajie ladha mpya kabisa kutoka kwa Joh Makini mwaka huu.”

Kwa sasa Joh anafanya vizuri na wimbo wake  “Perfect Combo” akimshirikisha msanii aliyekuwa naye kwenye Coke Studio Africa 2, Chidinma kutoka Nigeria.  Alisema, “Perfect Combo ilitayarishwa na mtayarishaji wa Kenya R-Kay na tena niliurekodi katika kipindi cha mwisho wakati tunarekodi Coke Studio Africa Kenya. Tulikuwa na wimbo huo kwa muda hivyo tuliamua kwenda kufanya video Afrika Kusini na Justin Campos na kuitoa.”

Falz, anayeshiriki kwa mara ya kwanza kwenye kipindi hicho, ameshanyakua tuzo ya BET ya ‘Viewers Choice Best New International Act’ mwaka 2016 na pia ile AMVCA 2015 ya muigizaji bora kwenye vichekesho.

Akijiandaa kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye kipindi hicho mwaka huu, Falz alisema, “Ni mara yangu ya kwanza kwenye Coke Studio Africa na najua kuwa utakuwa wakati mzuri. Kuunganika na Joh Makini kutoka Tanzania, kunawapa mashabiki ladha mchanganyiko na pamoja na kuungana kwa tamaduni zilizoshiba. Nimefarijika kwa heshima niliyopata ndani na nje ya Nigeria. Kupitia Coke Studio Africa, ninatarajia kufanya kazi za ushirikiano ndani ya Afrika na ninapanga kutengeneza chapa ya kimataifa,” na kuongeza,  “Kenya ni pazuri  – ninafurahia na pia ninajifunza Kiswahili na ninaipenda lugha hii na sauti yake.”

Joh Makini na Falz watakuwa wenyeji wa ukurasa wa Facebook wa Coca-Cola Facebook Alhamis hii  (tarehe 8 Septemba)  kuanzia saa 8 mchana.  Usipitwe na matangazo ya moja kwa moja. Wataweza kuyajibu pia maswali yako kuhusu safari yao kimuziki. Watweet @CocaColaAfrica maswali yako kwa kutumia hashtags: #AskJohMakini #AskFalz #CokeStudioAfrica

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad