Mtaa Kwa Mtaa Blog

JESHI LA POLISI KUZINDUA MAJENGO YA OFISI ZA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO MKOANI MBEYA.

JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya linapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa kutakuwa na uzinduzi wa majengo ya ofisi za dawati la jinsia na watoto zilizopo Polisi kati Mbeya na kituo kidogo cha Polisi ilomba, uzinduzi huu utafanyika tarehe 30.09.2016 Ijumaa.

Majengo hayo ya ofisi za dawati la jinsia na watoto ni moja kati ya majengo yanayojengwa nchi nzima katika kutekeleza mpango mkakati wa kujenga miundo mbinu ya ofisi za dawati la jinsia na watoto unaofadhiliowa na UNICEF.

Hivyo wananchi mjitokeze kwa wingi katika kushuhudia tukio hilo muhimu na la kihistoria katika mkoa wetu wa Mbeya.

Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala
kauli mbiu:- Funguka tumia dawati la jinsia na watoto kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Imetolewa na.
Ofisi ya Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget