HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 20, 2016

DC KASESELA AONGOZA MASHAMBULIZI KUZIMA MOTO UWANJA WA NDEGE NDULI IRINGA


Moto mkubwa ulizuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa leo. Moto huo inasemekana ulisababishwa na uchomaji mashamba yaliyopo jirani na uwanja huo. Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao ungeweza kuteketeza vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na majengo. 
Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (pichani na fulana nyekundu) ambaye alishirikiana na kikosi cha zimamoto kuzima moto huo alisema lazima wananchi wajue kutenga mashamba yao na  kuzuia mioto kusambaa
"Kuanzia sasa yoyote atakaye sababisha moto kutoka kwenye shamba lake atachukuliwa hatua kali za kisheria", alisema Mhe. Kasesela. 
Mkuu wa wilaya huyo piaaliagiza manispaa itengeneze kwa kutumia bullodozer barabara ya kuzuia moto kuzunguka uwanja. Moto huo ulianza majira ya saa 7 mchana na kusambaa hadi kwenye uwanja wa kuondokea ndege (Runway) na  kusogelea eneo la kuhifadhia mafuta ya ndege na vifaa vya kuongozea ndege. Ulidhibitiwa na Jeshi la Zimamoto vizuri na hadi kufikia saa 9.43 moto ulikuwa umezimwa.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiliongoza gari la kuzima moto kuelekea eneo la tukio la moto katika Uwanja wa ndege wa Nduli, Mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad