TAKWIMU zilizotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa
asilimia 96 ya wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John Pombe
Magufuli ikiwemo uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu bure.
Taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari na Mshauri Mwandamizi wa
Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema asilimia 88 ya wananchi wana imani
kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo mpaka mwisho wa awamu yake
ya kwanza ya uongozi.
Rais John Pombe Magufuli |
“Utafiti huu unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za Rais
za uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati asilimia 61 walipongeza sera ya elimu bure
wakati asilimia 61 walifurahishwa na usimamishwaji wa watumishi wa serikali”
alisema Chande.
Chande alisema kuwa katika utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na
hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika
huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni (asilimia
75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72).
Aliongeza kuwa kwa upande wa huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma,
utafiti unaonyesha kuwa asilimia 95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma
zinazotolewa na madaktari, walimu, na maofisa tawala katika ofisi za umma.
“Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi
wamesema suala la umakini na kanuni za demokrasia na haki ni vyema zifuatwe
ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji waondolewe pale tu
panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema Chande.
Akifafanua zaidi Chande alisema utafiti huo pia umeonyesha kubadilika kwa matarajio
ya wananchi ambapo katika kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni
mwa wananchi kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa watendaji. Na Daudi Manongi,
MAELEZO.
No comments:
Post a Comment