Mtaalamu wa upimaji wa saratani ya matiti kwenye banda la NHIF Dkt. F.Malibiche akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi waziri ofisi ya raisi (TAMISEMI), George Simbachawene (MB),takribani akina mama 113 na wanaume 5 waliweza kupimwa na kutogundulika na viashiria vya saratani.
Meneja
wa mfuko wa taifa wa bima ya afya, Fortunata Raymond akitoa taarifa ya
huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye banda la mfuko kwa Waziri ofisi
ya raisi (Tamisemi) Mhe.George Simbachawene MB.ambapo hadi sasa wanachi
na wananchama wa mfuko takribani 600 waliweza kupatiwa huduma za
upimaji.
Waziri
ofisi ya Raisi (TAMISEMI), George Simbachawene (MB) akisisitiza mfuko
kuendelea kupanua wigo wa elimu kwa wananchi waelewe faidia za kujiunga
na CHF ili kuongeza kasi ya uboreshaji wa huduma kama ilivyokusudiwa na
serikali ya awamu ya tano(5) kuwa ifikapo Juni, 2020 asilimia 30% ya
watanzania wawe wamejiunga na bima ya afya,mbele ya waandishi wa habari
wakati alipotembelea banda la NHIF katika maonesho ya nane nane
yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ngongo mjini
Lindi.anayemsikiliza mbele ni Meneja wa mfuko huo mkoa wa Lindi
Fortunata Raymond.
Waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene akipima BMI wakati alipotembelea banda la bima ya afya,wanaoshuhudia kulia mwenye kofia ya kijani Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi.

No comments:
Post a Comment