HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 12, 2016

ULEGA AENDELEA NA MCHAKA MCHAKA WA KUIPATA MKURANGA MPYA

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega amewaondoa hofu wananchi wake na kuwaeleza kwamba wasiwe na wasiwasi kwani Rais Dkt. John Magufuli anania njema na watanzania.

Ulega ametoa kauli hiyo katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Sotele kilichopo kata ya Dondo wilayani Mkuranga.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akimsikiliza Mganga wa Zahaniti ya Kijiji cha Sotele, Emily Bugingo wakati alipoitembelea katika kata ya Dondo bara, Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
 
Amesema kuwa hakuna haja ya kumchukia raia kwani anayoyafanya rais leo yamesababishwa na watu wachache ambao Kazi yao ilikuwa ni kujijali wenyewe tu na si vinginevyo. "Mnajuwa rais anadhamira ya dhati kabisa na watanzania na hasa katika bajeti ya mwaka huu ndio. maana fedha nyingi zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi hivyo kinachotakiwa nikumuunga mkono na kuzidi kumuombea tu." amesema Ulega

Akizungumzia maendeleo ya jimbo la Mkuranga alisema amejipanga kikamilifu kuwaletea maendeleo wananchi wake na ndio maana anapita kuwashukuru na kuhimiza maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibewa kilichopo kata ya Dondo, ambapo katika mkutano huo aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kisha akatumia fursa hiyo kusikiliza kero zao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Juma Abed akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Kibewa ambao aliwataka kumtumia Mbunge wao Ulega na kwamba ni muda wao sasa kumbebesha majukumu yao kwani ndio kazi waliyompa.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Kibewa Kata ya Dondo wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega (hayupo pichani).
Mbunge Abdallah Ulega wa Jimbo la Mkuranga akiwa sambamba na watendaji na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo akikagua mradi wa ufugaji wa samaki unaondeshwa na kikundi cha ufugaji samaki katika kijiji cha kibewa. (Picha na Emmanuel Massaka,Globuya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad