HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 4, 2016

Timu ya Vijana Serengeti Boys yawafata vijana wenzao wa sauzi, kukipiga jumamosi hii

Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini wakitokea Antananarivo, Madagascar walikoweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
Nyota wa timu ya Mpira wa Miguu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys na viongozi walipowasili Hoteli ya Garden Court Milapark ambako imepiga kambi kabla ya kuivaa Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye huo hapo mwakani. Serengeti Boys itakipiga na Afrika Kusini Jumamosi kwenye Uwanja wa Dobsonville, Johannesburg, Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad