HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 25, 2016

STARS YA MCHANGANI KUKIPIGA KESHO NA WA IVORY COAST UWANJA WA KARUME

Na Zainab Nyamka
KOCHA Msaidizi wa timu ya mpira wa miguu wa mchangani (Beach Soccer) Ally Sharif 'Adolph' amesema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kuweza kuhakikisha wanapita katika hatua hii ili kuweza kuingia kwenye fainali za mataifa Afrika mwezi Desemba.

Akizungumza kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho katika uwanja wa Karume, Jijini Dar es salaam, Adolph amesema wachezaji wote wapo vizuri na wameweza kuonyesha hamasa kuelekea mechi hiyo ambapo kama watafanikiwa kushinda wataingia moja kwa moja kwenye fainali hizo.

Timu hiyo inatarajiwa kukutana na Ivory Coast utakaopigwa majira ya saa 10 alasiri na utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Uganda.

Mwamuzi wa kati anatarajiwa kuwa Shafiq Mugerwa akisaidiwa na Ivan Bayige na Muhammat Senteza. Msimamizi wa muda akiwa Tsalaraza Maolidy kutoka Madagascar na msimamizi wa mechi ni Reverien Ndikuriyo Kutoka nchini Burundi.
Timu ya mpira wa miguu wa mchangani (Beach Soccer).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad