Waombolezaji wakilishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Marehemu Senga alifariki wiki iliyopita nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi AMIN.
Mjane wa Marehemu Joseph Senga, Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akiweka shada la Maua.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya FreeMedia wachapishaji wa Gazeti la Tanzania Daima alikokuwa akifanya Kazi Marehemu Joseph Senga, akitoa salamu za Rambirambi, wakati wa Mazishi yaliyofanyika Mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza.
Ibada ya Mazishi ikiendelea.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiweka shada la maua kaburini.
Mwili ukiwasili katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba Mwanza kwa ajili ya taratibu za maziko. (Picha na Said Powa)
Mama wa marehemu akisaidiwa kugusa mwili
wa mwanae kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Mke wa marehemu akigusa mwili wa mumewe kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Joseph Senga.
Mke wa marehemu Winfrida Senga akiweka shada la maua katika kaburi la mumewe, marehemu Joseph Senga.
Mtoto wa
marehemu, Joel Senga akiweka shada la maua.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Free Media, Neville Meena akiweka shada la maua.
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe akiweka udongo katika kaburi la marehemu.
Mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania
Daima, Marehemu Joseph Senga ukiwekwa kaburini wakati wa maziko yake
yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.
No comments:
Post a Comment