HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 1, 2016

MRI, CT-SCAN ZAPIGA MZIGO SAA 24 MUHIMBILI, WAGONJWA 41,101 WAPIMWA

Na John Stephen, MNH
 HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016 kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.

“Hospitali inahakikisha kila mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari.

 Mgonjwa akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Flora Lwakatare akifuatilia mgonjwa anavyochukuliwa vipimo leo mchana katika hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad