Mchezaji Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 .
(Picha na Selemani Semunyu).
Na Selemani Semunyu JWTZ.
TIMU ya Mpira wa Pete (Netball) ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imerejesha heshima yake baada ya Kuwafunga mabingwa Watezi wa Michuano hiyo kwa Mpira wa Pete Uganda kwa magoli 29 kwa 27.
Katika Mchezo huo uliokuwa wa Vuta nikuvute na rabsha za hapa na pale zilizizojitokeza kabla wakati na Baada ya Mchezo huo ambao ulikuwa na Upinzani Mkali kutokana na historia ya Timu hizo.
Katika Robo ya Kwanza Tanzania ilimaliza ikiongoza kwa magoli saba kwa Sita huku Timu zote zikicheza Mchezo wa kuviziana lakini uliojaa nguvu na kukamiana miongoni mwa Wachezaji.
Katika Robo ya Pili Tanzania pia ilimalizai ikiwa mbele kwa mabao 13 kwa 11 kukiwa na tofauti ya magoli mawili tofauti na robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa tofauti ya goli moja.
Robo ya Tatu Uganda walikuja na kusawazisha na kasha kuongeza na hivyo kumaliza kwa ushindi wa magoli 20 kwa 19 ya Tanzania na kuwafanya Tanzania kwenda kujiuliza.
Hatimaye robo ya Mwisho ikamalizika na Timu ya Tanzania kuibuka na Ushindi na hivyo kuwatisha Mabingwa wa mwaka uliopita pengine utarejea kwa Tanzania Kwa Upande wa Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema mechi yao na Uganda wamecheza kama fainali kutoka na historian a kuahidi kujipanga kwa ajili ya kuwakabili Kenya.
Kwa upande wake Nahodha Uganda Lilian Ajio amelalalimika Waamuzi kutoelewa Sheria Mpya za Mchezo huo hali iliyopelekea wakati mwingine kutokuwa na maamuzi sahihi.
Mchezaji
Faraja Malaki wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda
katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za
Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania
ilishinda 29-27 .
Mchezaji
Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa
Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za
Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania
ilishinda 29-27.

No comments:
Post a Comment