Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini
Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo
hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye
viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo
kesho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.
Alipowasili
ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey
Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.
Katika
Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe mara baada ya kuwasili mkoani Lindi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu wakati wa mapokezi na Vijana wa mkoa wa Lindi .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ndogo mkoani Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kwene Ikulu ndogo mkoani Lindi wengine pichani ni Waziri wa Kilimo Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe.Hamad Rashidi (kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa.






No comments:
Post a Comment