DALADALA lenye
namba za usajili T274 DEX, lililokuwa likifanya safiri zake kati ya Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke
jijini Dar es Salaam, limepiga mweleka mita chache tu kutoka kituo cha Daladala
Sabasaba-Mbagala mapema leo asubuhi (Agosti 11, 2016) na kujeruhi watu kadhaa.
Mashuhuda
wanasema, Daladala hilo lililokuwa katika mwendo kasi, liliserereka na kuacha
njia wakati likikaribia kusimama kituoni hapo.
Dereva
wa Daladala hilo aliruka na kukimbia, nakuwaacha abiria wakitaharuki kila mmoja
akijaribu kukoa maisha yake.
“Unajua
mvua hizi zilizonyesha asubuhi zinafanya barabara iteleze na hawa jamaa mwendo
wao unajua tena, sasa alijaribu kufunga breki gari likaanza kuserereka na
alipojaribu kurudi barabarani likakataa na kutumbukia mtaroni,” anasimulia
mmoja wa mashuhuda aliyekuwa eneo la ajali.
Polisi
wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya
kuliondoa gari hilo zilianza.
Abiria
wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia
kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.
HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
Wapita njia wakimuuliza abiria huyu (aliyekaa), ambaye alikuwa ndani ya daladala hilo
Polisi wa usalama barabarani, akikagua mazingira ya ajali hiyo huku akizungumza na simu yake ya mkononi
Mtu huyu ambaye haikujulikana maramoja kama ni muhudumu wa daladala hilo au abiria akitoka ndani ya daladala hilo baada ya "kupiga mwereka'
Mashuhuda kama kawaida yao









No comments:
Post a Comment