Wazee wa kijiweni katika eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam wakipata kikombe cha kahawa huku pembezoni kukiwa na lundo la uchafu lililotolewa kwenye mtaro kama ilivyokutwa na kamera ya yetu.
Mdau wa Mbagala akiwa katika harakati za kutafuta chupa kwa ajili ya biashara. Watu mbalimbali wamejiajili wenyewe kwa kufanya biashara za kuuza chupa tupu.
Mfanyakazi wa usafi akitimiza wajibu wake katika harakati za kuliweka jiji safi katika eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
Mama lishe akipika chapati kwa ajili ya wateja wake jirani na rundo la taka katika eneo la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijijni Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

No comments:
Post a Comment