Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Stella Rwezaura (katikati) mara baada ya kutembelea wodi ya wagonjwa ya Mwaisela mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za zilizozaagaa kwenye mitandao ya kijamii za mgonjwa Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani) aliyelazwa katika wodi hiyo anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) kulazwa chini katika wodi hiyo kutelekezwa bila kupatiwa matibabu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto) akipitia kwa makini jalada (file) la matibabu Bi. Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani) anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) kujiridhisha juu ya matibabu yake kufuatia taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii leo kuwa mgonjwa huyo ametelekezwa bila kupatiwa matibabu na kulazwa chini katika wodi hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kushoto) akiwa ameongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi kufuatilia ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo jijini Dar es salaam kuangalia ubora wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) juu ya huduma za Tiba alipotembelea wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumza na akina mama wenye watoto waliokuwa katika wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo.Amewahakikishia akina mama hao kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za Afya katika hospitali zake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akimsalimia mtoto aliyekuwa amelala na akina mama wenye watoto aliowakuta katika wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo kukagua ubora wa huduma za Afya.







No comments:
Post a Comment