HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 10, 2016

DAR FESTIVAL KUFANYIKA MWEZI SEPTEMBA LEADERS CLUB

Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbu wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipokuwa akielezea kuhusu Tamasha la Dar Festival linalotarajiwa kufanyika mwezi Septemba kwenye viwanja vya leaders Club Kinondoni jijini Dar es salaam lengo likiwa kutangaza utamaduni wa mtanzania, Kushoto katika picha ni Shabaan Kapilima Mkurugenzi wa Huduma Dar Festival na Katikati ni Faridi Faradji Mkurugenzi. Faridi Faradji Mkurugenzi wa Dar Festival akifafanua jambo wakati alipokuwa akielezea mipango mbalimbali juu ya maandalizi ya Tamasha la Dar Festival linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji na kushoto ni Shabaan Kapilima Mkurugenzi wa Huduma Dar Festival. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad