HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 10, 2016

Chama Cha Kuogelea chatembeza bakuli la mchango kuipeleka timu nchini Canada, Milioni 71 zahitajika

 Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), kinahitaji dola za Kimarekani 32,500 (Sh 71 milioni) kwa ajili ya kuipeleka waogeleaji nane (8) wa timu ya Taifa kwenye mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Windsor, nchini Canada.

Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka alisema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania inakuwa na jumla wachezaji 11 ambapo kati ya hao, wachezaji watatu watalipiwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina).

Namkoveka  alisema kuwa kila muogeleaji anatakiwa kulipiwa ni dola za Kimarekani 4,100 (Sh 8.2 million). Alisema kuwa TSA kwa sasa haina fedha za kuweza kuwapeleka wachezaji wote hao kwa ajili ya mashindano hayo.
Bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea nchini, Sonia Tumiotto akiwa katika mashindano ya Taifa kwenye bwawa la Hopac.

 Kwa mujibu wa Namkoveka, gharama kubwa kuipeleka timu  na kuwaomba wadau wa mchezo huo kuwasaidia ili kuweza kufanikisha lengo lao ka kuipeleka timu hiyo katika mashindano hayo.

“Tunahitaji kupeleka waogeleaji wengi zaidi katika mashindano haya ambayo ni makubwa duniani, mchezo wetu unakuwa kwa kasi na tunahitaji kupata waogeleaji wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa,” alisema Namkoveka.

Alisema kuwa TSA kimeunda kamati ya watu… kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inakwenda kwenye mashindano hayo.
Waogeleaji katika staili ya 'kuchupa' au Diving.

 Alisema kamati hiyo unaundwa na Mkurugenzi wa Fedha wa TSA, Phillip Saliboko, Asma Hilal, Amina Mfaume (Mkurugenzi wa Ufundi wa TSA), Inviolata Itatiro (Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club),  Geetha Prashant , Hamisi Mhini na Katibu Mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro.

Wachezaji waliochaguliwa kuunga timu hiyo ya Taifa ni Hilal Hilal, Aliasghar Karimjee, Ammaar Ghadiyali, Denis Mhini, Adil Bharmal, Joseph Sumari  ambao watashiriki kwa upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake ni Catherine Mason, Sylvia Caroiao, Sonia Tumiotto, Mariam Foum na  Magdalena Moshi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka akizungumzia maandalizi ya timu ya Taifa mbayo itashiriki mashindano ya Dunia yaliyopngwa kufanyika nchini Canada Mwezi Desemba.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Magdalena Moshi (wa tatu kutok kushoto) na Hilal Hilal (Wa pili kutok kulia) wakiwa na kocha wao, Alex Mwaipasi (wa pil kushoto) wakiwa na wanamichezo wengine wa Tanzani mjini Rio De Janeiro, Brazil kwa ajili ya michezo ya Olimpiki. Wachezaji hao wawili ni miongoni mwa waogeleaji 11 watakao iwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia mwezi Desemba nchini Canada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad