Bondia anaeiwakilisha nchi ya Namibia katika Mashindano ya Olimpiki yanayoendelea huko mjini Rio, Nchini Brazil,
Jonas Junias akijikuta akiingia hatiani na kujikuta akiswekwa rumande kwa tuhuma za Ubakaji, akidaiwa kumlazimisha kimapenzi, muhudumu wa chumba katika kambi ya wanamichezo.
Polisi nchini humo wanasema kuwa alimbusu mhudumu huyo bila ridhaa yake na alimuahidi kumpa pesa kama atakubali kufanya nae
mapenzi.
Hali kama hiyo pia inamkabili, Bondia wa Morocco, Hassan Sada aliekamatwa siku ya Ijumaa iliyopita kwa kosa la namna hiyo. Bondia huyo alikanusha tuhuma hizo lakini bado yupo chini ya usimamizi wa polisi.


No comments:
Post a Comment