
Ghorofa
lililojengwa ndani ya hifadhi ya reli maeneo ya Kamata jijini Dar es
salaam likiwekewa alama ya X na pia mmiliki wa jengo hilo alikabidhiwa
Notisi ya kulibomoa ndani ya siku 30.
Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini Julai 4, 2016 imeanza kutoa notisi ya siku 30 kwa watu waliovamia hifadhi za reli sambamba na kuweka alama ya X kwa wale wote waliokiuka na kuvamia hifadhi hizo.
Sheria ya reli ya mwaka 2002 kifungu cha 57 kinasema mita 15 kutoka kwenye reli pande zote mbili ni hifadhi ya reli kwa maeneo ya mjini na mita 30 kwa maeneo ya vijijini.
Tayari RAHCO ilitoa tangazo kwenye vyombo vya habari April 25, 2016 linalowataka wale wote waliovamia hifadhi za reli bila kuwa na vibali vya kuyaendeleza maeneo hao waondoke mara moja maana wamekiuka sheria hiyo ya reli. RAHCO haitahusika na gharama yoyote kwa wale watakaokiuka agizo la kuondoka kwenye hifadhi baada ya siku 30 za notisi.
RAHCO imeendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuitunza na kuijali miundombinu ya reli.
Zoezi hili la kuweka alama ya X na kutoa notisi limeanzia Dar es salaam na kuendelea maeneo yote ambako reli imepita katika mikoa yote.
Wafanyakazi wa RAHCO wakiwa na askari polisi wakati wa kuweka alama ya X katika kituo cha mafuta cha GAPCO kilichopo karibu na mtaa wa Lugoda na Kamata jijini Dar es salaam
Mwanasheria wa RAHCO Bw. Petro Mnyeshi akiwa na polisi kuhakikisha usalama wakati wa kuweka alama ya X na kuwasainisha notisi wakazi wa Buguruni Madenge baada ya nyumba zao kupimwa na kuonekana zipo ndani ya hifadhi ya reli
Wafanyakazi wa RAHCO, mwakilishi kutoka ofisi ya mipango miji Ilala na polisi wakipima eneo la hifadhi ya reli ili kuwawekea alama ya X waliovamia sehemu ya jengo la Mohamed Enterprises lililopo mtaa wa Lugoda ambalo ni moja ya majengo yaliowekewa alama hiyo na kupewa notisi ya siku 30 wawe wamebomoa
Majengo mengi yamekutwa ndani ya hifadhi ya reli ambapo kisheria lazima iwe mita 15 nje ya hifadhi kwa mijini.
No comments:
Post a Comment