HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 26, 2016

TCAA YAPATA TUZO ZA UBORA KIMATAIFA.

Na mwandishi wetu.
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepokea tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi ubora wa kimataifa, jijini Rome Italy Julai 25, 2016.

Kutolewa kwa tuzo hiyo  kunafuatia mashindano yaliyohusisha zaidi ya makampuni 300 duniani  ambayo yamesajiliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) na kupitia mchakato wa kupigiwa kura na hatimaye kupata washindi.

Meneja wa udhibiti wa viwangoTCAA, Magesa Sarota akielezea kuhusu tuzo hiyo alisema pamoja na mambo mengine  mashindano hayo yanaangalia  kampuni husika ni kwa namna gani inahakikisha inaendelea kutoa huduma zenye viwango katika masuala ya Uongozi pamoja na kuwa na mifumo inayohakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi viwango.

Tuzo hiyo ya TCAA ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari kwa niaba ya Mamlaka. Kupokelewa kwa tuzo hiyo ni heshima kwa Mamlaka na ni motisha ya kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya wa kimataifa.
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari  akionyesha  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa baada ya kukabidhiwa, jijini Rome Italy.
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) baada ya kukabidhiwa  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa na Raisi wa kampuni ya Otherways, Charbel Tabet inayoendesha mashindano hayo, jijini Rome Italy.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akiwa amepozi na  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa  jijini Rome Italy.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad