Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji(TIC),Clifford Tandari(kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Uwekezaji nchini Poland, Bartlomies Pawlak(kushoto) wakitia saini ya Makubaliano baina ya nchi mbili hususan katika Sekta ya Kilimo na kusaidia katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda pamoja na Elimu hapa nchini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Dkt Adelhelm James Meru
akizungumza na Wawekezaji mbalimbali wa Tanzania na Poland kuhusu
uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Gedfrey Simbeye akizungumza na Wadau wa Sekta ya Uwekezaji wa Tanzania na Poland juu fursa ya Uwekezaji iliyopo hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji(TIC),Clifford Tandari akiwasilisha mada katika mkutano huo uliowahusisha wadau wa Sekta ya uwekezaji wa Tanzania na Poland.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Uwekezaji wakisikiliza baadhi ya mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
No comments:
Post a Comment