HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2016

sikukuu za Eid na Sabasaba zasababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sikukuu za Eid al Fitr na Sabasaba zilisababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara na kuathiri wa baadhi ya shughuli za maendeleo.

Hatua hii ilitokana na wamiliki wengi wa ‘deport’ za mafuta kufunga kwa ajili ya kushiriki sikukuu hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano (EWURA) Bw.Titus Kaguo wakati wa mahojiano na Idara ya Habari(MAELEZO) wakati akitoa ufafanuzi juu ya uhaba wa tatizo hilo katika Mkoa wa Mtwara lililoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Alisema kuwa hivi sasa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo imerejea kwani vituo vingi vimeanza kuuza nishati hiyo baada ya sikukuu hizo kumalizika.

Bw.Kaguo alisema kuwa kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu binafsi na wahusika hao kushiriki sikukuu hiyo ilisababisha kusimama kwa shuguli hiyo, hatua ilivifanya baadhi ya vituo kukosa nishati ya mafuta na kushindwa kufanya kazi katika kipindi hiki cha sikukuu.

Aidha amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa nishati ya Petroli na Dizeli ipo kwa wingi kwani kwa siku ya jumanne dizeli lita milioni (5) tano ziliuzwa ukilinganisha na matumizi ya nchini ya siku ambayo ni lita milioni 4.8 na kwa Petroli lita zilizouzwa ni milioni 3.6 ukilinganisha na matumizi ya nchi nzima ya petroli ya lita milioni 2.8. kwa siku.

Aliongeza kuwa toka jumanne vituo kama Lake Oil,Tsn na Central belt vimeendelea kutoa huduma kama kawaida kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara.

Mji wa Mtwara siku ya Jumatano ulikumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na hivyo kufanya wakazi wa mji huo kununua nishati hiyo kwa bei ya ulanguzi toka lita shilingi 1950 hadi kufikia shilingi 2500 kwa lita jambo liloathiri shughuli za maendeleo ya wananchi.Habari
Na Daudi Manongi - MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad