HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 21, 2016

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AONYA UHUSIANO WA KINGONO KATI YA WAALIMU NA WANAFUNZI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo, amewataka waalimu wenye tabia ya kujihusisha katika mahusiano ya kingono na wanafunzi wao, kuacha mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaatarisha ajira na maisha yao.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua madarasa ya kidato cha tano na sita (5 -6) katika shule kongwe ya Sekondari ya Mdabulo iliyopo katika kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo akizindua kuanza kwa madarasa ya kidato cha 5-6.

Mh. Jaffo amesema, katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano Mwalimu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu za maadili ya mtumishi wa umma sanjari na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na kubainisha kuwa tayari zaidi ya Waalimu 10 wamebainika na kuadhibiwa.

Aidha, Waziri Jaffo ameuagiza uongozi wa halmashauri na Wilaya hiyo kusimamia haki na sitahiki za waalimu Wilayani huo ikiwepo kero sugu ya kutopandishwa madaraja inayolalamikiwa na waalimu nchini kote na kuangeza kuwa, kwa kutatua kero zao, itawajengea hali na shauku ya kufanya kazi kwa bidii hivyo kuinua kiwango cha elimu nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo alipowasili katika hospitali ya Wilaya Mafinga.

Shule ya Sekondari Mdabulo imeanza rasmi kutoa elimu ya juu ya sekondari  kwa wanafunzi wa kike pekee wapatao 70 kupitia michepuo ya HGL na HKL.

Pamoja na uzinduzi huo, naibu waziri JAFO alifanya ziara katika Zahanati ya Idunda, chamzo cha maji katika mji wa Mafinga, kukagua  utoaji huduma na kuzindua ufanyaji kazi wa mashine mbili za Ultra sound katika Hospitali ya Mafinga kisha akahitimisha kwa kuzungumza na watumishi wa Halmshauri za Mufindi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo akizungumza na umati wa wanafunzi na wazazi katika shule ya Sekondalri Mdabulo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad