Ghala moja lililokuwa linatumika kwa kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto jioni ya leo, chanzo cha moto huo inadaiwa kuwa ni mataili chakavu yaliyokuwa yakichomwa moto. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka tunaingia mitamboni, kikosi cha kuzima moto na uokoaji kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo.
Ghala likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego
Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea.
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Ghala hilo.
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Ghala
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa














No comments:
Post a Comment