Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Mkuu
wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) alipokuwa akimfafanulia
jambo kuhusu masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. IGP Kachama na ujumbe wake
yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri
Mwigulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest
Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Mkuu wa
Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) wakati wa ziara yake nchini
pamoja na ujumbe alioambatana nao walipokutana na Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es
Salaam, kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. Kushoto ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimuaga Mkuu wa
Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama mara baada ya mazungumzo yao
ofisini kwake jijini Dar es Salaam. IGP Kachama yupo nchini kwa ziara ya kikazi. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment