Moto umezuka na kuteketeza Kiwanda cha Nguo cha 21st Century au Polister kilichopo maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro asubuhi hii, chanzo cha moto huo bado hakijafahamika mpaka sasa na pia haijafahamika ni hasara kiasi gani imetokea kiwandani hapo na jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda vichache vinavyofanya kazi ambapo kwa sasa kilikua kinatengeneza khanga na vitenge tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julias K. Nyerere.
Moja ya Gari la Jeshi la Polisi likiwa katika jitihada za kuuzima moto huo.
No comments:
Post a Comment