JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa mapato kutokana na nyaraka hizo kutumika.
Watu hao wamekuwa wakitengeneza nyaraka ambazo ni vyeti vya kuzaliwa ,Cheti cha Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita, vyeti vya kuhitimu, Kadi za bima mbalimbali pamoja na mihuri mbalimbali ya taasisi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa watu hao wanawahoji juu ya watu walionufaika na vyeti bandia.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi (CP), Simon Sirro akiwaonesha waandishi wa habari nyaraka za
serikali bandia,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka.
Kamanda Sirro amesema kuwa watafatilia watu wote wenye vyeti bandia ambao watatajwa na wameajiliwa na serikali katika sehemu mbalimbali.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ashrafu Maumba (37) Mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) Mkazi wa Mnyamani pamoja na Mahamudu Zuber (24) Mkazi wa Buguruni.
Nyaraka walizowakuta nazo ni vyeti bandia vya kidato cha nne 50, stika za SUMATRA 20, Vyeti vya Vyuo vya Uuguzi, Vyeti vya Kuzaliwa 10, VETA 10, Cheti cha Darasa la Saba, Siri au Rakili bandia za vyeti vya CBE 10. Leseni za Biashara, nyaraka za bima 100 pamoja na nyaraka za COMESA 100.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la
Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hapo
pichani) kuhusu Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za
kutengeneza nyaraka za serikali bandia na kuisababishia serikali kukosa
mapato,leo jijini Dar es Salaam
Katika upekuzi huo waliweza kukamata mihuri mbalimbali ya Ofisi za Serikali na Binafsi, Muhuri wenye nembo ya bibi na bwana, Karatasi maalum zilizo na nembo za TRA kwa ajili ya kutengeneza kadi za vyombo vya moto Zaidi ya 500, Computa nne, Monitor Screen tatu, printer tatu Generator moja na stabilizer moja.
Baada ya uchunguzi watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Wakati huo huo jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki aina ya Short Gun Pump Action ikiwa na risasi sita pamoja na pikipiki aina Fekon .
Silaha na pikipiki hiyo walikamata wakati majambazi walikuwa wakitaka kwenda kuvamia na jeshi la polisi lilipata taarifa na kutumia mbinu zao za kuwakamata baada ya kuwakimbiza na kuweza kuacha vitu hivvyo.Na Chalila Kibuda.
No comments:
Post a Comment