Serikali imeitaka kampuni ya Dodsal Hydrocarbons kuongeza kasi
ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nchini
ili kuendana na mipango ya Serikali ya kuhakikisha kuwa nishati
hiyo inatosheleza mahitaji ya nchi kipaumbele kikiwa ni kuzalisha
nishati ya umeme.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam alipokutana na
Ujumbe wa kampuni hiyo ulioongozwa na mmiliki na Mwenyekiti
wa kampuni husika, Dkt. Rajen Kilachand. Kampuni hiyo inatafiti
mafuta na gesi kwenye eneo la nchi kavu katika Bonde la Mto
Ruvu mkoani Pwani.
“ Hatutaki kuchelewa, tunataka gesi ya kutosha ya kukidhi
mahitaji yetu kipaumbele kikiwa ni kuzalisha nishati ya umeme,
kutumika viwandani na majumbani, na ikitoshelesha mahitaji yetu
itatuwezesha pia kuzalisha umeme ambao tutauuza nje ya nchi,
lakini pia baadhi ya nchi barani Afrika zimeonesha nia ya kununua
gesi hii kutoka nchini,”alisema Profesa Muhongo.
Ujumbe wa kampuni hiyo ambayo mwezi Julai, 2015 ilitangaza
kugundua gesi ya kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.17 katika Bonde
la mto Ruvu, ulikuja kuonana na Profesa Muhongo ili kueleza
mpango kazi wa shughuli zake hapa nchini.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Dkt. Kilachand aliwashukuru
watendaji wa Wizara na TPDC kwa kushirikiana na kampuni
husika katika kuhakikisha shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi
na mafuta zinafanikiwa na kueleza kuwa kampuni hiyo inathamini
ushirikiano ulipo kati ya nchi za Tanzania na India na kuahidi
kuuendeleza kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa
katika kikao na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, (kulia) na
Ujumbe kutoka kampuni ya Dodsal Hydrocarborns (kushoto) inayofanya
shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Kikao
hicho kilijadili utekelezaji wa shughuli za kampuni hiyo nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki na Mwenyekiti wa kampuni ya Dodsal Hydrocarborns inayofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nchini, Dkt. Rajen Kilachand (kushoto). Dkt. Kilachand na Ujumbe wake walifika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini ili kuzungumzia utekelezaji wa shughuli za kampuni hiyo nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka kampuni ya Dodsal
Hydrocarborns inayofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na
gesi asilia nchini mara baada ya kumaliza kikao kilichojadili utekelezaji wa
shughuli za kampuni hiyo nchini. Kulia kwa Waziri ni Mmiliki na Mwenyekiti
wa kampuni hiyo, Dkt. Rajen Kilachand na Watendaji wengine ni
Shajee K.C (wa kwanza kulia), Salim Ajib (wa pili kulia), na Dkt.
Jogendra Sahu (wa kwanza kushoto).
Mmiliki na Mwenyekiti wa kampuni ya Dodsal Hydrocarborns, inayofanya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia nchini, Dkt. Rajen Kilachand (kushoto) akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kumaliza kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia). Kikao hicho kilijadili utekelezaji wa shughuli za kampuni hiyo nchini.
No comments:
Post a Comment