HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2016

BANDA LA MFUKO WA GEPF LAWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WAJASIRIAMALI KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABA SABA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu, Mh. Jenista Mhagama akizungumza na maafisa wa GEPF wakati alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 (Sabasaba) Jijini Dar es salaam, na kupatiwa maelezo ya jinsi Mfuko ulivyofanikiwa kutoa huduma kwa wajasiriamali.
Mh Jenista Mhagama akitia saini kitabu cha kumbukumbu za wageni waliopita katika banda la GEPF.
Uzinduzi wa Boda boda Scheme ulivutia wadau wengi wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara baada ya kupata maelezo ya mafanikio ya Boda Boda Scheme kutoka kwa Afisa masoko Bw Valence Masebu.
wajasiriamali (Mama lishe) wakijaza fomu za kujiunga na mpango maalum wa kujiwekea akiba ya uzeeni (VSRS) huku wakipatiwa maelezo na Afisa Masoko Bw Avit Nyambele.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad