Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Ayoub Nyenzi amekana kujiengua na klabu hiyo kama vyombo vya habari vinavyosema hasa baada ya kutofautiana na moja ya viongozi wakati wa ugawaji wa mapato ya Uwanja kati ya mechi ya Kimataifa ya Yanga dhidi ya Medeama ya nchini Ghana.
Akizungumza na Globu ya Jamii, Nyenzi amesema kuwa kauli yake ilichukuliwa sivyo na vyombo vya habari kwani yeye alikuwa anatetea maslahi ya watendaji wengine na hata hivyo suala hilo lilimalizika baada ya kesho yake kufanyika kwa mgawanyo huo wa mapato na kila mmoja kupata stahiki zake. "Ni kweli nilisema kauli hiyo hasa baada ya kuona ule utaratibu uliokuwa umepangwa wa kila siku wa mgawanyo wa fedha pale pale uwanjani kushindikana na kushindwa kuelewana na kufikoa kusema vile ila kwa kila kitu kipo sawa,".
Amesema, kwa sasa anaendelea na majukumu yake ya ujumbe wa kamati ya utendaji na hajaandika barua yoyote ya kusema kuwa anataka kujiengua katika klabu ya Yanga ila zaidi amewataka wana Yanga wote wawe na imani nae.
Nyenzi amesisitiza na kusema kuwa yeye bado ana majukumu ndani ya klabu ya Yanga na amewaomba wanachama kuendelea kumuamini kwani pale alikuwa anawatetea ila kwa sasa yameshaisha waendelee kuijenga timu.
No comments:
Post a Comment