Leo tarehe 30.6.2016 ndiyo tarehe na siku ya mwisho wa zoezi la kuhakiki silaha. Kwa
mujibu wa takwimu za silaha tulizonazo inaonyesha kwamba wapo baadhi ya wamiliki
wa silaha ambao hawajatekeleza agizo la kuhakiki silaha wanazozimiliki.
Kufutia hali hiyo, natoa angalizo kwa wale wote ambao hawajahikiki silaha zao
kwamba muda wowote kuanzia sasa tutaanza operesheni maalum ya kutafuta silaha
ambazo hazijahikikiwa. Ifahamike kwamba yeyote atakaye kutwa na silaha ambayo
haijahakikiwa atachuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza sifa ya kuwa
mmiliki halali wa silaha hiyo.
Tunatoa agizo kwa wamiliki binafsi wa maghala ya silaha waziwasilishe silaha hizo
pamoja na nyaraka zake katika vituo vya karibu vya Polisi kwa ajili ya uhakiki.
Imetolewa:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi
No comments:
Post a Comment