HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2016

Ubalozi wa Japan nchini wazindua rasmi Umoja wa wanameli ya viongozi vijana chapta ya Tanzania

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida amezindua rasmi Umoja wa wanameli ya viongozi vijana chapta ya Tanzania yaani Ship for World Youth Alumni Association of Tanzania [SWYAA Tanzania]. ‘Ship for World Youth Leaders [SWY]’ ni programu ya kimataifa inayolenga vijana ulimwenguni kote inayoendeshwa na serikali ya Japan.

SWYAA Chapter ni jukwaa linalolenga kuwaleta pamoja washiriki wote walioshiriki awali programu ya Meli ya Viongozi Vijana (SWY) na programu zinazofanana chini ya serikali ya Japan. Lengo kuu ikiwa ni Uongozi na ushirikiano katika maisha ya kila siku pamoja na kujitolea katika shughuli za maendeleo ya nchi husika.

Programu ya “Meli ya Viongozi Vijana”, inayoendeshwa na serikali ya Japan inahusu kushirikisha vijana kutoka nchi ya Japan na nchi mbalimbali duniani. Washiriki hupanda na kuishi pamoja kwenye meli huku wakijadili na kujifunza mambo mbalimbali yanayoikabili dunia na jamii zao kwa ujumla. Pia hupata fursa ya kushirikiana huku wakijifunza tamaduni mbalimbali za nchi tofauti tofauti huko melini. Programu hii iliyoanza mwaka 1988 imetimiza safari yake ya 25 mwaka 2013

Kihistoria Meli hii ya Viongozi vijana imewahi kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam mara mbili ikiwa ni mwaka 1996 na 2001.

Katika hotuba yake, Raisi wa SWYAA nchini Tanzania, Benedict Kikove amemuhakikishia Balozi wa Japan kwamba SWYAA –Tanzania itakua msingi imara kwa vijana wengi zaidi nchini kushiriki katika nyanja mbalimbali za Uongozi na shughuli za jamii kwa ujumla.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida na Rais wa Heshima wa SWYAA chapta ya Tanzania akiwa ameshika Katiba ya SWYAA chapta ya Tanzania pamoja na Rais wa SWYAA chapta ya Tanzania, Benedict Faustine Kikove.
Rais wa SWYAA Chapta ya Tanzania, Benedict Faustine Kikove akitoa hotuba mbele ya Balozi wa Japan, wanachama wa SWYAA na wageni waalikwa.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua rasmi wa SWYAA-Tanzania.
Katika tabasamu kubwa, wakiwa kwenye picha ya pamoja na balozi wa Japan baada ya uzinduzi rasmi wa SWYAA-Tanzania.
Wakiwa na nyuso za furaha, pichani ni wanachama wa SWYAA-Tanzania pamoja na Balozi Mdogo wa Japan nchini Tanzania, Hiroyuki Kubota.( Aliyeshikilia picha mstari wa mbele).
Maafisa wa ubalozi wakisikiliza kwa umakini hotuba kutoka kwa Balozi wa Japan.
Wadada mahiri viongozi wa leo na kesho na pia washiriki wanachama wa Meli ya Viongozi Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na balozi mdogo Ubalozi wa Japan, Mheshimiwa Hioroyuki Kubota.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad