Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
ZIKIWA zimesalia siku saba kwa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza(FDL) pamoja na daraja la pili(SDL) kuweka wazi wachezaji wanaowaacha kuelekea msimu ujao wa ligi kwa mujibu wa kalenda iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa Miguu nchini(TFF) inaonesha kuwa kuanzia Juni 15 hadi 30 timu hizo zinatakiwa kuweka wazi wachezaji wanaowaacha kwani jambo hilo ni muhimu ambalo linaweza kuwapa fursa timu nyingine kusajili wachezaji waliotoka ndani ya timu hizo kama wanawahitaji.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas (Pichani) amesema kuwa hadi sasa hakuna timu iliyotoa majina ya wachezaji waliowaacha kwani siku zilizobaki ni saba tu hivyo timu zinazishiriki FDL na SDL zinatakiwa kufanya zoezi hiyo mara moja kabla ya juni 30.
Amesema baada ya kumalizika kwa mapumziko yaliyomalizika Juni 10 kipindi kilichofuata ni usajili kilichofunguliwa Juni 15 huku kikitarajiwa kumalizika Julai 30. "Kwa mujibu wa Kalenda tuliyoitoa inazitaka timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15 hadi Juni 30 ili kuwapa fursa ya kuchukuliwa na timu nyingine", amesema Alfred.
Akizungumzia timu kutoka Ligi kuu timu zilizoshuka daraja ambazo ni Coastal Union, African Sports na Mgambo JKT zote za Jijini Tanga amesema kuwa katika ratiba pia iliyotolewa timu hizo zimewekwa makundi tofauti huku kila kundi likibeba timu nane. Huku kundi A likiundwa na timu za Abajalo ya Dar es Salaam, African Sports ya Tanga, Ashanti United ya Dar es Salaam, Kiluvya United ya Pwani, Friends Rangers ya Dar es Salaam, Lipuli ya Iringa, Mshikamano FC ya Dar es Salaam na Polisi Dar ya Dar es Salaam
Kundi B lina timu za JKT Mlale ya Ruvuma
Coastal Union ya Tanga, Kimondo FC ya Mbeya, Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam Kurugenzi ya Iringa, Mbeya Warriors ya Mbeya, Njombe Mji ya Njombe na Polisi Morogoro ya Morogoro na Kundi C linabeba timu za Alliance Schools ya Mwanza, Mgambo Shooting ya Tanga, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya Dodoma, Polisi Mara ya Mara, Rhino Rangers ya Tabora na Singida United ya Singida.
No comments:
Post a Comment