HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 21, 2016

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MGENI RASMI MAONESHO YA TAASISI ZA KIFEDHA JULAI 27, JIJINI DAR

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya taasisi za kifedha  (benki)  na kiuchumi  yatakayofanyika Julai 27 hadi 29 mwaka huu, Mlimani City jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya  Imori International ambao ndio waandaaji wa Maonyesho hayo, Leo Nyanduga amesema kuwa maonyesho ni kwa ajili ya wananchi kutambua umuhimu wa benki  katika kusaidia ukuaji wa uchumi kutokana na fursa zinazozalishwa na benki na taasisi za uchumi.

Nyanduga amesema  katika maonyesho hayo  fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo, mipango ya uwekezaji,  pamoja na  changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kukaa pamoja na kujua ni kwa jinsi gani wanaweza kuzitazama  na kuzitatua changamoto hizo.

Amesema  maonesho ni  kuangalia nafasi  ya kuinua maisha ya wananchi katika kuhakikisha wanafaidika kupitia taasisi  za kifedha  katika kuweza kukopa na kuweza kuwekeza  katika miradi mbalimbali.

 Nyanduga amesema  ni asilimia ndogo ya Watanzania ndiyo wamekuwa wakitumia huduma za kibenki kutokana  na kukosa elimu ya kutosha ya faida za kutumia sekta za benki na uwekezaji katika soko la hisa, lakini kupitia Maonyesho hayo ya Taasisi za Kibenki 2016 wengi watafaidika.

Amesema  wananchi watapata nafasi ya kupata elimu na kukutana kwa karibu na  watumishi wa mabenki, soko la hisa, vicoba, microfinance, huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu na kujenga ukaribu ili kuhakikisha wananchi wanatumia kikamilifu huduma zao katika kusaidia ukuaji wa sekta ya fedha nchini.

Nyanduga ameeleza kuwa maonyesho hayo ya sekta za kifedha na uchumi yaliyodhamiria kuwa chachu kuu ya kukutanisha benki  zote, taasisi zote za kifedha, taasisi zote zinazoweza kutoa huduma mbalimbali kwenye sekta hiyo, yatakuwa ni mwanzo wa kukuza zaidi sekta hiyo kikamilifu.

Amesema maonyesho yaleta chachu katika sekta, kuwapa nafasi watu kujua namna taasisi hizi za kifedha zinavyoweza kutatua changamoto zao wakizitumia vyema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad