HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA NAIBU WAKE WAKUTANA NA WANANCHI ANA KWA ANA NA KUTATUA KERO ZA ARDHI

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kupitia watendaji wake wakuu leo tarehe 21/06/2016 amefanya utaratibu maalumu wa kukutana na wananchi wenye kero na migogoro ya ardhi.

Katika kutekeleza hilo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka wamekutana na wananchi ana kwa ana ili kuwasikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero na migogoro yao inayohusu ardhi na nyumba.

Hatua hii imefuatia baada ya hapo jana tarehe 20/06/2016 viongozi hao kukutana na watumishi wa Wizara hiyo na kutatua kero zao zinazohusu maslahi ya watumishi ambapo kwa mwaka huu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameamuliwa yafanyike kwa utaratibu huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila Akiwakaribisha wananchi walio na kero za migogoro ya Ardhi ofisini kwake ili kuzitatua kero zao ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka (katikati mwenye suti na tai) akipokea kero za wananchi zinazohusu migogoro ya Ardhi ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad