Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony Mavunde (kushoto), akipokea
msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 6 kutoka kwa Mkurungenzi
wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi yaliyotolewa na benki hiyo kwa
ajili ya Shule ya Msingi Makole iliyopo Manispaa ya Dodoma,mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na
Vijana), Anthony Mavunde (wa pili kushoto), akifurahi pamoja na wanafunzi wa
Shule ya Msingi Makole iliypo manispaa ya Dododma mara baada ya
makabidhiano ya msaada wa madawati 50 uliotolewa na wafanyakazi wa Benki
ya CRDB tawi la Dodoma, wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,
Dk. Jasmin Tsekwa (wa pilikulia) na kulia ni Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la
Dodoma, Rehema Hamisi.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma
wakiwa wamekaa kwenye madawati ambayo waliikabidhi shule ya msingi makole
iliyomjini Dodonma jana ,msaada huo unathamani ya zaidi ya sh milioni 6.
Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma Rehema Hamisi (kulia)
akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliyopo mjini Dodoma, baada
ya kuwakabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa wa benki
hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali kupunguza tatizo la madawati
mashuleni.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Dodoma, Rehema Hamisi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi ya Makole Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony Mavunde akioa hotuba yake wakati wa hafla ya kupokea madawati 50 yaliyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole Dodoma.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kuimba kwaya.(Na Mpigapicha Wetu)
No comments:
Post a Comment