HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 27, 2016

NIMEMALIZA MKATABA NAA COASTAL UNION NIPO HURU KWENDA KOKOTE- HUMUD.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIUNGO wa Coastal Union Abdulhalim Humud (Pichani)amesema yeye ni mchezaji huru na anaweza kukaa mezani na timu yoyote kwa sasa kwani mkataba wake na Coastal Union umekwisha kwa sasa huku timu hiyo ikiwa tayari imeshashuka daraja.

Akizungumza na Michuzi Blog Humud amesema kwa atakayehitaji huduma kutoka kwake basi watakaa mezani na kuingia makubaliano nao na kuweka wazi changamoto alizokutana nazo katika timu ya Coastal Union mpaka kupelekea kushuka daraja na chanzo kikuu kikiwa ni ubovu wa uongozi uliopo pale.

"Nimemaliza mkataba wangu na Coastal Union na nipo huru kujiunga na timu yoyote kwa sasa na watakaonihitaji nitakaa nao mezani na kuweka makubaliano kwa kila upande kuridhika na makubaliano hayo,"amesema Humud. Kiungo huyo ameweka wazi matatizo yaliyopo kwenye timu ya Coastal Union na kusema viongozi ndiyo wamefanya mpaka timu hiyo kushuka daraja kwani wameshindwa kuiongoza kipindi chote na hata chama cha mpira wa miguu mkoa nao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana.

Amesema, wamekuwa na kikosi kizuri sana katika ligi ila wakashindwa kujituma sana kwani walikuwa hawapati stahiki zao kama inavyotakiwa na kuishia kucheza mpira wakiwa wameshavunjika moyo na kuona bora liende.

Humud amewahi kukipiga katika timu za Simba na Azam na baadae Sofapaka ya Kenya na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu alizopitia katika kipindi chote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad