HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AAGIZA MABADILIKO MAKUBWA IDARA YA UHAMIAJI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameagiza yafanywe mabadiliko makubwa katika Kitengo cha Upelelezi kwa watendaji wa Mkoa wa Dar es salaam ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.

Masauni ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara.  Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma .

Katika kikao hicho, Masauni ameagiza watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji Kitengo cha Upelelezi katika Mkoa wa Dae es salaam wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wahamishwe na kupelekwa katika maeneo mengine nchini.

Aidha ameagiza pia kuwa kuanzia sasa watumishi waliohudumu katika idara hiyo kwa muda mrefu katika kituo kimoja wahamishiwe maeneo mengine ili kuboresha utendaji wa kazi wa idara hiyo.

Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya hiyo ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.

"katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa" Alisema Masauni.

Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wizara hiyo kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ya kazi na waepuke vitendo vya kupokea rushwa na uzembe kazini.

kuhusu Utaratibu wa Ajira za Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Masauni amesema kuwa Serikali inapitia upya utaratibu wa ajira katika Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama yaliyopo katika Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi ili kuhakikisha kuwa wanaojiriwa katika vyombo hivyo ni wale tu wenye sifa zinazostahiki

Pia ameagiza Idara ya Uhamiaji kuandaa Mpango mkakati ambao ni kabambe ili kuthibiti wimbi la wahamiaji haramu hapa nchini

Kuhusu matukio ya uhalifu yaliyojitokeza hivi karibuni amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua za haraka ikiwemo uchunguzi wa matukio hayo ambapo tayari watumiwa kadhaa wamekwisha kukamatwa kuhusiana na matukio hayo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad