
Njia hii imekuwa ikipendwa sana kutumiwa na ndugu zetu waendesha Bodaboda, kwa madai kwamba hiyo ni njia nyepesi zaidi kwao kwa safari zao. Lakini njia hiyo si yao na wanafahamu fika matumizi ya njia hiyo, lakini bado wao wanaendelea kujiachia tu, kana kwamba hawafahamu lolote au ni njia iliyotengenezwa kwa matumizi yao.
Ni hivi karibuni Mabasi hayo yaendayo haraka yameanza kufanyiwa majaribio katika njia hizo, ila cha kushangaza kama si chakustaajabisha ni pale ndugu zetu hao wa Bodaboda wanapoendelea na matumizi ya njia hiyo, na wakati mwingine kulazimisha kutaka kulipita hata basi hilo katika sehemu ambayo hata ujiti hauwezi kupita.
Jambo hili yapaswa kuangaliwa kwa jicho kali sana, maana kama vijipu upele hivi vitaendelea kuwepo, basi kuna siku vitakuja kuwa vidonda vikubwa na vishindwe kutibika.
No comments:
Post a Comment