HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 24, 2016

KIBOKO ALIYETISHIA MAISHA YA WATU AULIWA KIJIJI CHA MAGUNGA, IRINGA


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wananchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi hao wa kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. 

Kiboko huyo alijificha kwenye eneo ambapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipatikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake. 

Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi​
Mmoja wa Maafisa Wanyaka pori akitoa maelezo kwa wananchi kabla ya kwenda kufanyika kwa zoezi la kumdhibiti Kigoko huyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwambatana na baadhi ya wananchi na Maafisa Wanyama Pori kuelekea aliko Kiboko huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa maelekezo wakati wa kumtoa Kiboko huyo baada ya kuuliwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad