HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 23, 2016

KIBADENI AMEWATAKA VIONGOZI WA SIMBA WAWAPENI NAFASI VIJANA ILI WANAWEZE KUWASAIDIA.

Kocha wa zamani wa timu ya Simba Abdallah Kibadeni.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KOCHA wa zamani wa timu ya Simba Abdallah Kibadeni ameutaka uongozi wa Simba kukiangalia zaidi kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya timu yake kinachonolewa na Mganda, Jackson Mayanja kwani kama wakiamua kukiangalia kwa muda huu kuelekea msimu ujao wanaweza kuwa na mafanikio kutokana na uwezo waliouonesha.

Kibadeni amesema Simba imebadilika sana kwani kwenye mchezo wa mwanzo  amekutana nayo na siyo ile aliyoizoea inayokuwa na mchanganyoko na wachezaji wakubwa, kikosi hicho kimeonesha mchezo mzuri na uliotulia licha ya kushindwa kutumia vema nafasi walizozipata.

"Endapo viongozi wa timu hiyo wanataka kuwa na timu yenye ushindani basi ni vema kikosi hicho wanatakiwa kukiangalia kwani nina imani itakuwa miongoni mwa timu zitakazokuwa na kikosi tishio,"amesema Kibadeni. Katika mchezo dhidi ya timu yake Simba hawakuwa na kitu cha kupetoteza na walikuwa uwezo mkubwa wa kumaliza wakiwa nafasi ya pili.

"Simba wamecheza mpira mzuri sana lakini naweza kusema goli letu la kwanza limeweza kuharibu mipango yao kwa kiasi kikubwa", amesema Kibadeni na dakika zote 90 Simba wamecheza mpira mzuri ukilinganisha na walivyokutana nao katika mechi za awali.

Kibadeni amesema matokeo waliyoyapata hayakuwazuia kupambana na hata walipopata goli kupitia kwa nahodha wake Musa Mgosi lakini wakaendeleza mashambulizi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad