HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 27, 2016

JTI wazindua mradi kupunguza ajira kwa watoto

Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaharu Yoshida(kulia) akimpongeza kwa kumshika mkono Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu, Dk. Abdallah Possi mara baada ya kuzindua Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaharu Yoshida, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa ya kuzindua Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.
Mkurugenzi wa miradi ya jamii Duniani kutoka JTI(Global Director,Social Programs), Elaine McKay, akizungumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu maamlumu ya Arise yenye lengo la kuelimisha jamii kupiga vita Ajira kwa Watoto katika Sekta ya Kilimo iliyozinduliwa Mkoani Morogoro juzi.

Na mwandishi wetu, Morogoro

KAMPUNI ya Sigara ya JTI Tanzania imezindua mpango mpya uitwao ARISE wenye lengo la kupunguza ajira kwa watoto kwenye sekta ya kilimo.

ARISE ambapo kwa kirefu inamaanisha (Achieving Reduction of Child Labor in Support of Education) ni mradi endelevu wa miaka mingi ulioanzishwa nchini Brazili na Malawi kwa ajili ya Jamii ambapo zinajiusisha na shughuli za kilimo cha Tumbaku.

Lengo kuu la mpango wa ARISE ni kutatua changamoto za kiuchumi na za kijamii zinazopelekea wakulima wadogo wadogo wa tumbaku kuwafanyisha kazi watoto wadogo kwenye mazingira hatarishi. 

 Mpango huu umeundwa kuongeza upatikanaji wa elimu nzuri kwa watoto, kuongeza ufahamu kuhusu athari za ajira kwa watoto, kuboresha mazingira na maisha ya jamii ya wakulima wa tumbakuhususani kwa jamii ya wakulima ambao JTI wanafanya biashara nao pamoja na kushirikiana na halmashauri pamoja na serikali za mitaa kwenye sheria za kazi.

Akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika Mkoani Morogoro juzi, Rob Glenn, mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya sigara ya JTI, alisema: “JTI inaelewa vyema umuhimu wa jamii ambazo zinahusika katika ukulima wa Tumbaku; tunaheshimu sana mchango wao katika maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi". Glenn alisema kuwa ajira kwa watoto ni janga kubwa nchini Tanzania na hizi ajira zinapelekea athari kubwa sana kwa afya za watoto, usalama wao na pia zinaweza kuwa na madhara makubwa ya kisaikolojia.

Aliongezea kuwa mojawapo ya mambo makubwa yanayopelekea uwepo wa janga hili ni pamoja na umaskini, kutofatiliwa kwa sheria zinazopinga ajira kwa watoto, matatizo na vizuizi vya watoto kupata elimu na changamoto nyingine nyingi.

"Elimu ni kitu muhimu sanakwenye hili suala la ajira kwa watoto. Na kwa kupitia mpango wa ARISE tunategemea kutakua na upungufu mkubwa wa tatizo la ajira kwa watoto," alisema.

 Aliongezea kuwa kwa mara ya kwanza, Mpango wa ARISE ulianzishwa nchini Malawi na Brazili kupitia ushirikiano kati ya Winrock International (WI) - wakalawaliobobeakwenyemasuala ya kilimopamoja na shirika la kazi duniani(ILO)hukuikiwashirikishajamii, serikali za mitaapamoja na halmashauri Akizungumzia ushiriki wa ILO kwenye mpango wa ARISE , Mary Kawar Mkurugenzi mkuu wa ILO nchini Tanzania alisema: “Tumefurahishwa na kuridhishwa na kampuni ya TCC kwa Kujikita kwenye huu muungano uliopelekea uwepo wa mpango wa ARISE.

Lengo la mpango wa ARISE nimuendelezo wa mipango yetu ya muda mrefu ya kupunguza ajira kwa watoto kwenye sekta ya kilimo hususani kwenye kilimo cha tumbaku”.

Kwa hivi sasa mradi wa ARISE utakuwepo kwenye vijiji vitatu vya Uyui, Urambo na Kaliua mkoaniTabora. Kwa Tanzania hivi vijiji vitatu vitatu ni mradi wa majaribio na huu mradi utakapofanikiwa utaendelea kwenye vijiji vingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad