HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2016

HATUNA TAARIFA YA TCHECHE WALA HATUJAPOKEA BARUA KUTOKA ZAMALECK WALA - YANGA.

Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
UONGOZI wa Yanga umekana taarifa za kuwa timu ya Zamaleck ya nchini Misri kuleta ofa ya kuwataka wachezaji wake watatu na kusema kama watapata barua kutoka huko hawana budi kukaa mezani nao.

Akizungumza Katibu Mkuu wa Yanga  Baraka Deusdedit (Pichani)amesema ameshapokea simu za watu wakimuuliza kuhusiana na hilo lakini ukweli kuwa hawajapata barua yoyote kutoka Zamaleck na kama kweli wanawahitaji wachezaji basi watakaa mezani na kukubaliana. Taarifa zinazosambaa ni kuwa Zamaleck wametuma barua ya kuwataka Golikipa Deogratius Munish 'dida', Juma Abdul na Vicent Bossou.

"Nimesikia kwa baadhi ya watu na wengine wamenipigia simu juu ya hilo kuwa wachezaji watatu wanatakiwa na Zamaleck na tayari wameshatuma barua na kusema kuwa uongozi wa Yanga umeshapokea na suala liko mezani,"amesama Deusdedit. Nataka niwahakikishie tu mashabiki wa Yanga kuwa suala hilo halipo na wao kama sekretarieti hawajapokea ila litakapofika watapata taarifa kwani mpira ni kazi.

Akijibu suala la usajili wa mchezaji wa Azam, Kipre Herman Tcheche amesema kuwa hana taarifa hiyo na anazidi kushangaa kuona taarifa hizo zinasambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kudai."Nasikia tu kuwa Yanga wamemsajili Tcheche lakini sina taarifa hizo kwa sasa na zaidi mimi ndio mtendaji Mkuu wa Yanga suala lolote lazima lije mezani kwangu,"amesema Deusdedit.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad