Beki wa Timu ya Yanga, Haji Mwinyi akimtoka Mchezaji wa timu ya APR ya nchini Rwanda, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1, na kuifanya timu ya Yanga kuendelea na mbio za mashindano hayo, huku timu ya APR ikiyaaga baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Rwanda.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG
Kiungo wa Timu ya APR, Yannick Mukunzi akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa kwa ustadi mkubwa, lakini haukuza matunda baada ya beki wa Yanga, Vicent Bossou kuuzuia, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.
Nahodha wa Timu ya APR, Iranzi Jean Claude, akichuana vikali kuwania mpira na Mshambuliaji wa Pembeni wa Yanga, Deus Kaseke, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe, akionyesha umahiri wake wa kuwachambua mabeki wa Timu ya APR, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.
ahodha wa Timu ya APR, Iranzi Jean Claude, akiwasalimia Washabiki wa timu ya Yanga, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment